Thursday, August 25, 2016

CUF YA TANGANYIKA NA CUF YA ZANZIBAR!

 Na Hamidu Bobali.

Sikusudii kujibu mapigo lakini ni vyema kujikumbusha. Nimestaajabu sana kilichoandikwa na gazeti la Jambo Leo kuhusu hatma ya chama chetu, yakinukuliwa maelezo ya Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama, Bi. Magdalena Sakaya.

Hoja za kukizushia chama chetu kuwa ni:
1. Chama cha Waislamu,
2. Chama cha Waarabu,
3. Chama cha Zanzibar,
4. Chama cha wapemba,
5. Chama cha Maalim Seif,

Zote zilikuwa ni propaganda chafu zilizoenezwa na CCM wakitumia kitengo cha propaganda cha usalama na miaka yote zimekuwa zikigonga mwamba na chama kinazidi kuchanja mbuga.

Leo haya ni mapyaaa! Hoja hizi kushabikiwa na kiongozi wa ngazi ya juu wa chama, Naibu Katibu Mkuu, ambaye chama hiki kimemuamini na kumpa ubunge wa viti maalum akitokea serikalini mwaka 2005 - 2010, akapewa ubunge wa viti maalum mara ya pili na chama hiki mwaka 2010 - 2015, akagombea ubunge jimbo la Kaliua, Tabora, akaungwa mkono na ushirikiano wa UKAWA, akawa mbunge wa kuchaguliwa 2015 - 2020.

Uzanzibar na ubara si ajenda ya chama chetu hata Siku moja, agenda zetu siku zote ni kuwaunganisha watanzania. Leo hii kusikia Maneno haya kutoka kwa kiongozi wangu wa juu nimefadhaika sana. Sijui ni nini kimempeleka kwenye mitego hii.

Yawezekana kiongozi wangu hajui " core objective of our party", "The civic united Front " Kutugawa wazanzibar na wabara sisi watu wa maeneo ya pwani huku maana yake ni kutuachanisha undugu, nje ya siasa sisi ni ndugu

Wito wangu kwa wana CUF wote, TUSIKUBALI KUGAWANYIKA KIRAHISI RAHISI NAMNA HII

Hamidu Bobali (MB),
Mwenyekiti JUMUIYA YA VIJANA YA CUF (JUVICUF),
Mbunge wa Jimbo la Mchinga (CUF),
25.08.2016.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu