Thursday, August 11, 2016

DALADALA LAPINDUKA KITUONI MBAGALA-SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM, WATU KADHAA WAJERUHIWA

Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo.
Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo.
Wapita njia wakimuuliza abiria huyu (aliyekaa), ambaye alikuwa ndani ya daladala hilo.
Polisi wa usalama barabarani, akikagua mazingira ya ajali hiyo huku akizungumza na simu yake ya mkononi.
Mtu huyu ambaye haikujulikana maramoja kama ni muhudumu wa daladala hilo au abiria akitoka ndani ya daladala hilo baada ya "kupiga mwereka'
Mashuhuda kama kawaida yao.
HABARI/PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.

DALADALA namba T274 DEX,(pichani), lililokuwa likisafiri kutoka Mbagala RangiTatu kuelekea Temeke jijini Dar es Salaam, limeanguka mita chache kutoka kituo cha Daladala Sabasaba - Mbagala leo asubuhi Agosti 11, 2016 na kujeruhi watu kadhaa.

Mashuhuda wanasema, Daladala hilo lililokuwa katika mwendo kasi, liliserereka na kuacha njia wakati likikaribia kusimama kituoni.

Dereva wa Daladala hilo aliruka na kukimbia, nakuwaachaabiria wakitaharuki kila mmoja akijaribu kukoa maisha yake.

“Unajua mvua hizi zilizonyesha asubuhi zinafanya barabara iteleze na hawa jamaa mwendo wao unajua tena, sasa alijaribu kufunga breki gari likaanza kuserereka na alipojaribu kurudi barabarani likakataa na kutumbukia mtaroni,” anasimulia mmoja wa mashuhuda aliyekuwa eneo la ajali.

Polisi wa usalama barabarani alifika muda mfupi baada ya ajali hiyona taratibu ya kuliondoa gari hilo zilianza.

Abiria wote walitoka salama, wachache walijeruhiwa na baadhi yao walionekana wakilia kutokana na mshtuko wa ajali hiyo ya asubuhi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu