Malkia wa Tarabu nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jana baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw. Addo November, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila baada ya kumaliza kuswali alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali alikokimbizwa alikutwa amekwishafariki.

Kwa mujibu wa familia marehemu Bi. Shakila Saidi anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Agosti 20, 2016 saa 10 alasiri katika makaburi ya Uwanja wa Ninja huko Mbagala Charambe jijini Dar es salaam

Namna ya kufika msibani nyumbani kwa marehemu kwa kutumia daladala. Unapanda magari ya Mbagala Rangi Tatu, ukifika mwisho unachukua basi la Nzasa na unashuka Mnara wa Voda hapo unauliza kwa Bi Shakila utaonyeshwa.

KALALE PEMA PEPONI KIPENZI CHETU BI. SHAKILA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Mungu amlaze pema peponi bi Shakila saidi, binafsi sijawahi kumuona kwa macho, ila nilipenda sana itokee siku nimuone, nimeanza kumsikia zamani miaka ya sabini nikiwa mdoogo, sauti tamu maneno mazuri, niliposikia yuko jkt nilitamani itokee siku aje mkoa ninaoishi nimuone hata kwa wimbo mmoja lakini nikasikia amestaafu kuimba,
    naamini wengi hawakubahatika kumuona kwa macho ila wanapenda sana sauti na nyimbo zake, daima tutamkumbuka na kumuombea, binaadamu woote tuko njiani yeye ametutangulia tu na binaadam waliofanya mema wema wao ulikuwa kwetu sote poleni ndugu jamaa na marafiki sisi tuko nyuma yake.
    mola tumuombe amlaze pema peponi, amina

    ReplyDelete