Wednesday, August 31, 2016

MAONI YA MSOMAJI; WOSIA WANGU KWA WANAHABARI KUELEKEA SEPTEMBA MOSI

Tunaelekea siku ya Septemba Mosi siku ni ambayo wanasiasa nchini kama wanataka kututumia ngazi kwa maslahi yao ya kisiasa.

Nashauri mambo yafuatayo;

(1). Kamwe tusikubali kutumika ama kutumiwa kwa ajili ya kuwakweza wanasiasa kwa kuwa siku zote furaha yao imekuwa mauti yetu.

(2). Tufanye kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma yetu bila kushabikia upande wowote wa kisiasa ili kuwa salama kwa kuwa STORI nzuri ni ile itakayokuacha ukiwa HAI.

(3). Tutambue kuwa hata tukiwa kimbelembele namna gani siku hiyo hakuna tija wala maslahi tutakayopata zaidi ya kubaki na maumivu, majeraha na hata vifo na kuziacha familia zetu zikihangaika na wengine wakibaki wajane na yatima.

(4). Siasa sio kila kitu katika taaluma ya habari kwani tunaweza kuandika habari za kijamii zinazoweza kusaidia kuibua kero na matatizo ambayo hatimaye yatasaidia chachu ya maendeleo kwa jamii husika.

(5). Tutumie kalamu na kamera zetu kuwaangazia akina mama na watoto wanaokosa huduma za afya na baadhi yao kufa kwa kukosa dawa ama huduma nzuri katika vituo vya Afya.

(6). Tuibue na tutafiti sababu za kukwama kwa maendeleo katika maeneo yetu na kuwamulika watendaji wanaojifanya miungu watu ambao wanasababisha nchi yetu na wananchi wake waendelee kuwa maskini na kuishi kwa mlo mmoja kwa siku.

(7). Nasisitiza hatutasifiwa kwa kuwa kimbelembele kukaa kwenye taget na kulegwa shabaha kwa kudhani kuwa kwa kufanya hivyo tutasifiwa.

RASHID MKWINDA,
-MSHINDI WA NNE WA TUZO YA HABARI ZA RUSHWA NA UTAWALA BORA 2008/MAZINGIRA(2013).

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu