Saturday, August 20, 2016

MATUKIO YA MAZISHI YA BI. SHAKILA SAID HUKO MBAGALA CHARAMBE JIJINI DAR

Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala Charambe, jijini Dar,wa pili kushoto akishuhudia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Mbagala Charambe,jijini Dar,kushoto ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye.
Mke wa Rais Mstaafu awamu ya nne,Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala Charambe, jijini Dar.
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kulia) na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye (pili kushoto) wakishiriki maziko ya aliyekuwa Mkongwe, mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarabu hapa nchini,Bi Shakila Saidi ambaye mazishi yake yamefanyika leo huko nyumbani kwake Mbagala Charambe, jijini Dar.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu akijadiliana jambo na mmoja wa waombolezaji nyumbani kwa marehemu,kabla ya maziko kufanyika.Bi Shakila,amefariki ghafla nyumbani kwake,huko Mbagala Charambe.
Baadhi ya Waombolezaji wakiwa nyumbani kwenye mazishi ya Bi Shakila,aliyefariki ghafla nyumbani kwake, huko Mbagala Charambe.
Baadhi ya Waombolezaji wakiwa nyumbani kwenye mazishi ya Bi Shakila,aliyefariki ghafla nyumbani kwake, huko Mbagala Charambe.
Mwili wa marehemu Bi Shakila ukiswaliwa tayari kwa maziko
Waombelezaji wakiwa wamebeba Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Bi Shakila wakielekea mazikoni,jioni ya leo huko nyumbani kwake Mbagala Charambe, jijini Dar.
Mwili ya Bi Shakila tayari umeishapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele
Safari ya mwisho ya Bi Shakila Said.
Rais Mstaafu awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete (wa tatu kulia) akijalidiliana jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (pili kushoto).
Rais Mstaafu awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akizungumza na waombolezajiPicha zote na MMG.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu