Tuesday, August 2, 2016

MAZISHI YA JOSEPH SENGA KATIKA PICHA

Mwili ukiwasili katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba Mwanza kwa ajili ya taratibu za maziko. (Picha na Said Powa)
Mama wa marehemu akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na ndugu.
Mama wa marehemu akisaidiwa kugusa mwili wa mwanae kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.
Mke wa marehemu akigusa mwili wa mumewe kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.
Waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Joseph Senga.
Mke wa marehemu Winfrida Senga akiweka shada la maua katika kaburi la mumewe, marehemu Joseph Senga.
Mtoto wa marehemu, Joel Senga akiweka shada la maua.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Free Media, Neville Meena akiweka shada la maua.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima marehemu Joseph Senga wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza.
Ibada ya mazishi ikiendelea.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiweka udongo katika kaburi la marehemu.
Mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Marehemu Joseph Senga ukiwekwa kaburini wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza.
Ibada ya mazishi ikiendelea.
Wanafamilia wakiwa katika ibada ya mazishi katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu