Monday, August 29, 2016

MCHIMBA KISIMA AFIA NDANI YA KISIMA JIJINI ARUSHA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Na Woinde Shizza, Arusha.

Mchimbaji wa kisima aliyefahamika kwa majina ya Waziri Omary (25) mkazi wa Ngaramtoni amefariki dunia kisimani wakati akichimba kisimani.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amekiri kutokea kwa tukio hilo marehemu alikutwa amefariki kisimani baada ya kutumia moto wa mkaa.

Alisema marehemu huyo aliwasha moto wa mkaa kulainisha mwamba ili aweze kupata maji, Pia alisema kisima hicho akichokuwa anachimba chenye urefu wa futi 60, alikutwa saa 5 juzi akiwa ameshapoteza maisha.

"Kilichotokea ni kwamba huenda wakati amewasha jiko, Carbonmonoxide ilizidi huku hewa ya Oxygen ilikuwa ndogo kiafya lazima angedhurika , "alisema

"Mwili wa marehemu haujakutwa na jera lolote, tunaendelea na uchunguzi kubaini zaidi , "alisema Kamanda.

Pia amewatahadharisha watu kuhakikisha watu nawapotumia majiko ya mkaa ndani kuhakikisha kuna hewa ya kutosha.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu