Tuesday, August 23, 2016

MHAMASISHAJI MKUU WA CHADEMA ADAI KUTELEKEZWA NA UONGOZI

Mhamasishaji Mkuu wa Siasa za Chadema kwa njia ya nyimbo na sanaa Fulgency Mapunda akizungumza na waandishi wa habari huku akibubuji kwa na machozi
Mhamasishaji Mkuu wa Siasa za Chadema kwa njia ya nyimbo na sanaa Fulgency Mapunda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Agosti 21 kuhusu hatma yake ndani ya chama hicho.

NA MWANDISHI WETU

Mhamasishaji Mkuu wa Siasa za Chadema kwa njia ya nyimbo na sanaa Fulgency Mapunda amewataka viongozi wa wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Chadema) kumfahamisha hatima yake ndani ya chama hicho akiwa kama mhamasishaji mkuu wa Program za Chama kupitia siasa.

Aidha anawata viongozi hao wamfahamishe hatima ya Idara ya Sanaa ndani ya Chadema kama kitengo mahususi cha kuhamasisha Program za Chama kupitia sanaa.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam jana Mapunda alisema amefikia hatua hiyo
baada ya kutokea sintofahamu kati yake na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashindi.

Mapunda alisema tangu Mei mwaka huu imetokea sintofahamu kati yake na Dk. Mashindi kwa kufanya mageuzi ya kimfumo ndani ya Chadema.

“Figisufigisu hizi zinafanywa na wakurugenzi wanaomzunguka Katibu huyo, akiwemo John Mrema na Reginald Munishi dhidi yangu,”alisema Mapunda.

Mapunda alisema pamoja na umuhimu wa pekee wa Idara ya Sanaa katika kuhamasisha program za Chadema katika kutengeneza taswira chanya ya Chadema mbele ya macho ya umma, bado idara hiyo imefutwa na Katibu Dk. Mashindi.

“Swali langu kwa bwana Mrema na Munisi mbona mchujo huu haujawagusa kwa wale wenye mlengo wa kwao na walitumia vigezo gani kwa sababu karibu wote wamerudishwa na kuniacha mimi mwenye sifa, taaluma na uzoefu ,” alihoji Mapunda.

Mapunda alimtaka Mwenyekiti wa Chadema Taifa, na kamati kuu watambue mchango wake na kujua hatima yake ndani ya Chadema.

“Nataka nijue iwapo wamenitelekeza pamoja na ukweli kwamba tulikua pamoja siku zote za mapambano kwa miaka zaidi ya 15, tukipambana katika dhiki na raha,” alisema Mapunda.

Baadhi ya nyimbo alizotunga na kuimba kama mhamasishaji Mkuu wa Chadema ni Chadema Chadema Peoples Power, Tuyamwage Mafisadi , Operesheni Sangara, Wabunge wa Chadema Twende, Fagia uwanja utakate MBoe apite, Chadema Mwendo mdundo.

Nyingine ni Chadema tuko tayari,vua gamba vaa gwanda, kwa heri mafisadi, haturudi nyuma, chagua shangilia, chadema ni dara na Dikteta uchwara.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu