Saturday, August 27, 2016

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMSIMAMISHA KAZI AFISA MAENDELEO YA JAMII WA JIJI KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani J. Kihamia amempuzisha kutekeleza majukumu yake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji Bi. Mwantumu Dosi kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu yake hivyo kukiuka kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.

Mkurugenzi Kihamia ametoa taarifa hiyo leo tarehe 27.08.2016 baada ya kukamilisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kufanya tathmini ya miradi iliyopitiwa na Mwenge na kugundulika kwa dosari zilizojitokeza katika moja ya mradi ambao uko chini ya Idara hii.

Mradi huo ni kikundi cha vijana wanaojishughulisha na Uselemara pamoja na Uchomeleaji kinachojulikana kama Mbeshere Umoja Group kilichopo Kata ya Olorieni kiligundulika kuwa na wananchama waliovuka umri wa miaka 35 ambao hawastahili kunufaika na Mikopo ya Vijana kwa mujibu wa Sera.

Mwenge wa Uhuru katika Jiji la Arusha ulikimbizwa tarehe 24.08.2016 na Kikundi hicho kilikua ni miongoni mwa miradi iliyokua inapitiwa na Mwenge wa Uhuru ambapo wanachama wake hawakizi vigezo. Wanachama hao walikua wameandaliwa kupewa Hundi ya TSH Milioni tano kama ishara ya kuunga mkono jitihada zao zakuboresha maisha. Mkimbiza Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. George Jackson Mbijima alisitisha zoezi hilo baada ya kugundua dosari za umri kwa baadhi ya wanachama.

Kupumzishwa kutekeleza majukumu ya Mkuu wa Idara hii kunafuatana na masharti ya kukabidhi Ofisi kwa Mratibu wa Tasaf Bi. Tajiel Mahega ambaye kwa sasa atakua Kaimu Mkuu  wa Idara hii mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.

Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji la Arusha.
27 Agosti,2016

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu