NA MWANDISHI WETU.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni (DC), Ally Hapi, amewataka warembo wanaoshiriki shindano la Miss Kinondoni 2016 kuzingatia nidhamu ili kuepuka kuichafua fani hiyo mbele ya jamii, huku pia akiwapongeza waandaaji waliopanga kutoa asilimia 10 ya mapato kuchangia mfuko wa madawati wilayani humo.

Akizungumza na warembo hao waliomtembelea ofisini kwake juzi, Hapi alisema kuwa nidhamu ni jambo muhimu mno katika mashindao hayo ya urembo kwani ndiyo inayoweza kuyajenga au kuyabomoa.

“Mzingatie nidhamu, mjiamini na mjijengee uwezo wa kujieleza, hatutaarjii kusikia maneno mabaya ambayo yanaweza kulichafua shindano,” alisema na kusisitiza ni matarajio yake taji la Miss Tanzania litarejea Kinondoni kwani ndiyo wilaya yenye rekodi ya kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi.

Juu ya mpango wa waandaaji kutoa asilimia 10 ya mapato ya viingilio kuchangia madawati, alisema: “Kwa kufanya hivyo, mmemuunga mkono Rais John Magufuli katika harakati zake za kuboresha elimu nchini, lakini pia hii inaongeza thamani ya shindano lenu kuona mnasaidia wadogo zenu, name nitakuwapo siku hiyo.”

Mmoja wa warembo hao, alimshukuru kiongozi huyo akisema: “Tunashukuru sana kwa kukubali kutukaribisha ofisini kwako, lakini pia tukupongeze kwa kuteuliwa kuwa Mkoo wa Wilaya ya Kinondoni, tukiamini Rais Magufuli alifanya hivyo kutokana na kukuamini kupitia mpango wake wa kuwapa nafasi zaidi vijana.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rahimat Promotion, Rahima Yusuph, alimuhakikishia kiongozi huyo shindano lao la mwaka huu litakalofanyika Ceptemba 2, kumtoa Miss Tanzania kama ilivyo kawaida yao kutokana na ubora wa warembo walionao ambao wengi wanakidhi vigezo vya mashindano hayo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: