Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande katikati akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa soka barani Ulaya leo Jijini Dar es salaam, kulia ni Meneja Uendeshaji Ronald Baraka Shelukindo na kushoto ni Afisa Masoko Furaha Samalu.
---
Msimu mpya ya Ligi bora za soka ulimwenguni imewadia na kuanzia Jumamosi tarehe 13 Agosti, Ulimwengu wa Mabingwa, SuperSport, utawaletea mashabiki wa soka barani Afrika michuano yote moja kwa moja (Live) ya msimu mpya katika kiwango cha HD kupitia DStv!

Mashabiki wa soka mlipatiwa kionjo cha msimu ujao wa soka mwishoni mwa wiki iliyopita wakati DStv ilipoonyesha pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu la kugombea Ngao Ya Hisani ambalo lilishuhudia Man United wakitwaa kikombe cha kwanza mbele ya mabingwa wa Ligi Kuu Ya Uingereza msimu uliopita, Leicester City. Na kama shauku na mpagao wa msimu uliopita ni dalili ya chochote, basi msimu huu mpya wa Ligi Kuu Ya Soka Uingereza utakuwa sio wa kawaida huku mechi zote 380 zikipatikana kupitia DStv!

Kwa uhakika mechi zisizopungua 300 zitaonyeshwa moja kwa moja (Live) kitu ambacho kinathibitisha kwamba SuperSport ndio mpango mzima kwa wapenzi na watazamaji wa soka na matukio mengine ya kimichezo barani Afrika. Chaneli hii ya michezo hukuletea matangazo kwa mapana na marefu ambayo hujumuisha uchambuzi wa kina wa Premier League kutoka kwa wachambuzi mahiri wa soka ambao hawana upinzani kokote barani Afrika.

Msimu huu unaokuja utaleta kivutio kikubwa zaidi huku Premier League ikiwa na mechi za siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza. Hizi pia zitakuwa sehemu ya ofa kutoka SuperSport kwenda kwa mashabiki wa soka. Kama kawaida siku za Jumamosi zitaendelea kuwa za soka kwa mechi zinazoanza saa Kumi Jioni (4pm) kwa saa za Afrika ya Kati ambapo SuperSport itakuwa inarusha hadi michezo mitatu ya ziada kwa wakati mmoja kupitia chaneli mbalimbali za SuperSport SS3, SS5, SS6, SS7 na SS11. Chaneli maarufu ya Premier League ya masaa 24 itaendelea kuwepo kupitia SS11 kuendelea kuthibitisha kwamba SuperSport ndio makazi ya soka la kimataifa.

Kwa wapenzi wa soka la Ligi Kuu ya Uingereza, patakuwa na burudani mfululizo na bila kuchelewa kwani pia kutakuwa na wiki tano ndani ya msimu ambapo kutakuwa na michezo ya katikati ya wiki ambayo itarushwa katika siku za Jumanne na Jumatano.

Msimu unaanza Jumamosi tarehe 13 Agosti na kumalizika Mei 21, 2017.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: