Tuesday, August 30, 2016

MWANDISHI SIMON KIVAMWO ANAHITAJI DAMU KUOKOA MAISHA YAKE, SHIMYE WANAHABARI NA WADAU

Bw. Simon Kivamwo
Waandishi wa habari wakitoa damu ili kuwezesha matibabu ya Mwandishi wa habari mkongwe hapa nchini Bw. Simon Kivamwo ambaye anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Ocean Road iliyoko jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari anayeratibu zoezi hilo Bw.Thompson, Kivamwo ambaye anaugua kwa muda mrefu sasa, amezidiwa na maradhi leo hii na kukimbizwa kwenye hospitali hiyo ambapo madaktari walihitaji kumuongezea damu. 

Benjamin Thomspon ametoa wito kwa wanahabari na jamii kwa ujumla kujitokeza kumchangia damu mwandidhi mwenzetu ili kuokoa maisha yake. Sehemu ya kutolea damu ni Hospitali ya Mnazi Mmoja, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu