Friday, August 12, 2016

MZEE YUSSUF AACHANA NA MUZIKI WA TAARABU SASA KUHAMIA MSIKITINI

 Mfalme wa Muziki wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati, Mzee Yussuf leo ametangaza kuachana na muziki na kumrudia mwenyezi Mungu.

Mzee Yussuf ameitangaza hatua hiyo leo ijumaa Agosti 12, 2016 baada ya Muda mfupi baada ya kumaliza kuswali swala ya ijumaa katika msikiti wa Ilala Bungoni (Masjid Taqwa) huku akibubujikwa na machozi mengi.

Mzee Yussuf ameomba waumini wamuombee msamaha kwa Allah kwa kipindi chote alichokuwa amemuasi na kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo katika kutangaza na kusifia za bwana mtume muhammad (s.a.w).

Aidha amewaomba watu wote wenye Cd zake majumbani pamoja na vituo vya redio na televisheni kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba Kwa Allah.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu