#‎1. Aliyekuwa‬ Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ktk mkutano wa CUF na kuletea kusitishwa kwa mkutano huo.

‪#‎2. Akijibu‬ maswali kadhaa ya mwandishi wa Habari wa Azam Tv, Prof. Lipumba anasema ni kweli yeye kama mwenyekiti aliyejiuzuu hakualikwa wala hana vigezo vya kuingia ktk mkutano huo, lakini akiwa nyumbani alipata ujumbe wa simu ya mkononi kuwa anahitajika ukumbini na baadhi ya wanachama wanataka arudi katika nafasi yake.

‪#‎3. Baada‬ ya kupata ujumbe huo, Lipumba aliamua kuondoka nyumbani kwake na kwenda ukumbini,ambapo kimsingi kikatiba na kikanuni hakuwa na ruhusa ya kuingia, lakini kwa nafasi yake ktk chama alipaswa kuruhusiwa kuingia japo walinzi walimgomea wakisema haitajiki kwa muda huo, yeye alilazimika kuhakikisha anaingia ili kuweza kukidhi kiu ya wanachama waliomhitaji na wanaoona anafaa kurudia nafasi yake.

‪#‎4. Prof‬ Lipumba anasema hakuna mwana-CUF anayeijua CUF kama yeye na wala hakuna mwana-CUF toka Tanzania bara na hata visiwani ukitoa Maalim Seif aliyeweza kuwatetea Wazanzibar kama yeye, akitolea mfano wa kudai haki ya mwaka 2001 na harakati nyingine za kuwasemea na kuwatetea Wazanzibar. Lipumba anasema yeye ndiye kiongozi aliyezunguka Tanzania bara na visiwani na kufahamiana na viongozi wa ngazi zote na ndio hao wanaomtaka arudi katika nafasi yake.

‪#‎5. Akijibu‬ swali la kuwa "anatumiwa na Watu kuivuruga CUF", Prof Lipumba anasema hawezi kuihujumu CUF kwa sababu yeye ndio sehemu ya waasisi wa chama hicho na amekipigania kwa miaka mingi ndani ya jasho na damu, hivyo kuwataka viongozi wa CUF Taifa kutumia hekima na kuacha maamuzi ya wanachama wanaotaka yeye arudi na kuchukua nafasi yake na kuendeleza harakati za kuindoa CCM madarakani kuelekea 2020.

‪#‎6. Prof‬ anasema bado ana imani kuwa wanachama wanataka yeye arudi na ndio maana hata baada ya kuwa yeye si sehemu ya mkutano kikatiba na kikanuni, bado kuna wanachama walimpigia simu afike ukumbini na kujuwa hatima yake ya kurudia nafasi yake.

Source: Azam TV.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: