Friday, August 19, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMWAPISHA MKUU WA MKOA MPYA WA ARUSHA, MRISHO GAMBO IKULU JIJINI DAR

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo leo Agosti 19, 2016 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. Magufuli amemteua Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha baada ya kutengua uteuzi wa Felix Ntibenda katika mwendelezo wa mabadiliko madogo ya kuimarisha safu ya utawala wake.

Uteuzi wa Gambo unakuja takriban miezi miwili baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha mwisho mwa Juni mwaka huu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Ntibenda anahamishiwa katika ofisi yake kwa ajili ya kupangiwa majukumu mengine.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu