Wednesday, August 10, 2016

RC LINDI AZINDUA AWAMU YA PILI YA MRADI WA UUZAJI VIWANJA VYA UBIA KATI YA UTT - PID NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa viwanja vya ubia kati ya UTT-PID na halmashauri ya manispaa ya Lindi uliofanyika katika ukumbi wa Kagwa, Lindi.
Mkuu wa mkoa akikabidhi hati kwa mmoja wa wanunuzi wa viwanja vya mradi.
Wageni mbalimbali walioalikwa ndani ya ukumbi wa Kagwa kuhudhuria uzinduzi huo.
Wageni mbalimbali walioalikwa ndani ya ukumbi wa Kagwa kuhudhuria uzinduzi huo.

Mkuu wa mkoa wa Lindi amesifia utekelezaji wa mradi wa ubia wa viwanja kati ya Manispaa ya Lindi na Taasisi ya Miradi ya UTT- PID huku akizindua awamu ya pili ya utekelezaji ambapo itahusisha upimaji na uuzaji wa viwanja zaidi ya 8,000 katika maeneo tofauti ndani ya Manispaa ya Lindi.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa katoliki wa Kagwa pia uliudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Meya wa Manispaa, Wakurugenzi wakuu wa Taasisi Mbalimbali, wawekezaji na wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Elimu ya juu.

Uwasilishwaji wa maada juu utekelezaji wa awamu ya kwanza na mipango mikakati ya awamu ya pili ulifanyika kutoka pande zote mbili yaani UTT-PID and wataalamu toka Manispaa ya Lindi.

Akieleza kwa kina Meneja Miradi wa Manispaa alisisitiza Taasisi Mbalimbali zilizonunua awamu ya kwanza kuanza ujenzi mara Moja huku akidai halmashauri imetenga zaidi ya ekari 1,500 bure kwa Chuo chochote kitachokua tayari kuanza kuwekeza ndani ya kipindi kifupi kijacho.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu