Tuesday, August 30, 2016

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 235 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI KAGERA

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro akipokea msaada wa madawati 235 kwa mkoa wa Kagera toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande jana kwenye shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba.
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini Deodatus Kinawiro akihutubia wakazi wa Bukoba baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi Kagera makabidhiano hayo yalifanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba
Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande akitoa hotuba kwa wageni waalikwa na wanafunzi mara baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi za mkoa wa Kagera ,katika hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakishuhudia makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi mkoani Kagera toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakiwa wameketi kwenye moja ya dawati kuonyesha kuwa wamepokea madawati toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu