Thursday, August 4, 2016

UTT-PID NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI ZASHIRIKI PAMOJA MAONESHO YA KILIMO YA NANENANE, LINDI

Maofisa wa Taasisi ya miradi ya UTT wakiwa pamoja na watumishi wa Halmshauri ya Manispaa ya Lindi katika Maonesho hayo ya Nanenane.
Wateja mbalimbali kutoka ndani na nje ya Lindi wakipata maelezo juu ya miradi mbalimbali ya ardhi inayofanywa kwa ushirikiano kati ya wabia hao wawili
Moja ya Miradi mikubwa iliyofanywa na ubia huu ni upimaji wa viwanja katika eneo la Mabano na Mmongo, uuzaji na uwekaji wa Miundombinu ya barabara.

Kwa muendelezo wa ubia huo na mafanikio ya awamu ya kwanza ubia huo kati ya Taasisi hizo mbili za Serikali wataingia utekelezaji wa awamu ya pili ya upimaji na uuzaji wa viwanja katika maeneo tofauti ndani ya Manispaa ya Lindi.

Kupitia ubia huu na mapato Manispaa ya Lindi iliyopata iliwezesha wakazi wa halmashauri kunufaika na vitu vingi ikiwemo:

- Ujenzi wa maabara kwa shule za Sekondari.

- Ujenzi wa nyumba za walimu.

- Ujenzi wa nyumba za waauguzi.

- Ununuzi wa magari pikipiki na boti kama vyombo vya usafiri.

- Ununuzi wa trekta ya manispaa.

- Ukarabati na ununuzi wa fenicha ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri.

- Ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule zote za sekondari za halmashauri.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu