Thursday, August 18, 2016

UVCCM YACHANGIA KUNG'OLEWA KWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

Picha na maktaba aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Filex Ntibenda ambaye uteuzi wake umefutwa.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha na anatarajiwa kuapishwa kesho ikulu jijini Dar es salaam.

Na Woinde Shizza, Arusha.

Hatimaye mkuu wa mkoa wa Arusha Filex Ntibenda uteuzi wake umefutwa na Rais John Magufuli ambapo mkuu wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo ataapishwa kesho kuwa mkuu mpya wa Mkoa huo imefahamika.

Hata hivyo kuna ishara zote kuwa mvutano uliojitokeza kati ya mkuu wa zamani Ntebenda na UVCCM  mkoani hapa ndiyo ulioachangia kwa kiasi kikubwa RC huyo kung'olewa.

Uchunguzi wa weti unebaini kuwa sakata la wapangaji kulipa kiasi kidogo cha fedha katika mradi wa maduka ya UVCCM, mikataba mibovu na mkuu wa mkoa kumpigia simu katibu wa Uvccm Mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel akimtaka ache kuwabughudhi wapangaji kunatajwa ndiko kulikoiudhi ikulu na kufukuzwa kazi.

Jambo jingine ambalo pia linatajwa na wadadisi wa mambo ya kisiasa mkoani hapa ni mfululizo wa matukio ya uchomaji moto katika shule tano za sekondari huku RC akionekana kutochukua hatua muhimu za kuyakabili masuala hayo.

Mapema wiki ya juzi katibu wa Uvccm Ezekiel Mollel aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtaka aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Ntibenda aaache mara moja kumpigia simu za vitisho ili kuwalinda wapangaji wasiotendea haki uvccm katika malipo ya miradi yake badala yake ampigie simu za kupambana na hujuma, ufisadi aidha dhidi ya mradi ya chama au ile ya serikali.

Kwa upande wake mwenyekiti w a UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya naye alisema kuwa wanamshukuru Rais Wa nchi hii ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM taifa kwa kusikia kilio cha wana Arusha na kuamua kumtoa mkuu huyo wa mkoa na kuleta mwingine.

Napenda kuchukuwa nafasi hii kumpongeza rais wa nchi hiii kwa kumuona mkuu huyu wa mkoa kuwa ni jipu afai kwani kuna mambo mengi ambayo ameyafanya yasioyofaa tunamuhaidi kumuuunga mkono na kumpa ushirikiano wa kutosha mkuu mpya wa mkoa Mrisho Gambo" Alisema Sabaya.

Alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kumpa ushirikiano wa kutosha mkuu huyu wa mkoa kwani ni mchapakazi na pia ni mtenda haki.

Naye katibu hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emanueli Kiusa alisema kuwa wao vijana wa chama cha mapinduzi hawatakuli kuwa na kiongozi mzigo ,fisadi na ambaye anapenda rushwa na asiyesimamia haki na iwapo kama kunakiongozi wa namna hiyo ndani ya chama ajitoe mapema maana UVCCM wakimgundua hawata muacha.

Alisema kuwa anaamini mkuu mpya wa mkoa anatambua kazi aliotumwa kuwafanyia wananchi hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Arusha ,viongozi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa serikali kumunga mkono kwa kumpa ushirikiano ili aweze kufikisha mbali mkoa watu na kuwafanyia watu wa Arusha mambo makubwa ya kimaendeleo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu