Saturday, August 6, 2016

WAKAZI WA MANISPAA YA KINONDONI KUTIBIWA KWA KADI YA TIKA TIKA

 Mstahiki Meya wa Boniface Jacob mapema Agosti 5, 2016 amezindua huduma ya afya inayoitwa Tiba kwa Kadi katika manispaa yake.

Huduma hii ya TIKA iliyoanzishwa Kinondoni, inatakiwa kutolewa nchi nzima endapo mpango huu utafanikiwa kwa kupata mwamko wa wananchi kujitambua na kujikatia bima ya Afya kwa sh 40,000 kwa mwaka.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meya Jacob alisema kwamba safari ya kuanzisha TIKA haikuwa lelema lakini wanamshukuru Mungu sasa wamefika asilimia kubwa hata kuzindua.

"Tulitafuta ela huku na kule ili kufanikisha Azma yetu, kazi oliyobaki ni kwenu wananchi kuchangamkia fursa".....
Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akionyesha kadi ya kupewa huduma ya afya kwa tshs. 40,000/- tu kwa mwaka.
Mstahiki Meya Jacob akikagua mashine za kutengeneza vitambulisho.
Mstahiki Meya Jacob akiwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya Joh Makini aliyehudhuria hafla ya uzinduzi huo.
Mstahiki Meya Jacob akiwa na wasanii waliomuunga mkono.

" Nitawaomba sasa watendaji kutengeneza vipeperushi vingi ili viende katika Kata, Mtaa na katika hospitali zetu ili kuhamasisha watu kujiunga"alisema Meya Jacob

Alisema mpango wa manispaa hiyo ni kusajili watu laki 3 kwa mwaka na kuhakikisha inasajili wananchi wote milioni 1.9 hata kama wilaya zitagawajika.

Meya Jacob alisema kadi ya TIKA imewalenga sana wananchi wasio na sekta rasmi kama vile wajasiriamali, waendesha Bodaboda,mama na baba lishe, mafundi gereji na makundi mengine muhimu yaani wazee na walemavu.

"Huduma hii itamsaidia sana mwananchi kwani wenye magonjwa sugu ya malaria watahudumiwa vizuri, upasuaji mkubwa na mdogo na magonjwa yote ya wanawake na watoto TIKA Itahudumia.

Naye Naibu Waziri wa Afya Dk Hamis Kigwangala, alisifu manispaa hiyo kuanzisha huduma ya TIKA na kueleza kwamba kadi yako ndiyo tiba yako mwaka mzima.

Alisema, anatarajia kwamba fedha zitakazopatikana katika huduma ya TIKA zitaende kuboresha huduma hiyo kununua dawa na vifaa tiba na kuhakilisha huduma hiyo inapatikana bila shida.

"Azma ya serikali ya awamu hii ya tano ni kutoa huduma ya afya kwa asilimia 60...kwa maana nyingine wananchi wote nchini kuwa na kadi ya bima ya afya"

Imeandikwa na Janet Josiah.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu