Meneja wa kitengo cha Airtel Money , Asupya Naligingwa akiongea wakati wakuitambulisha huduma mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kuweza kuongeza pesa kwenye kadi zao za mabasi ya mwendokasi kupitia huduma za kifedha ya Airtel Money
Meneja wa kitengo cha Airtel Money , Asupya Naligingwa akiongea wakati wakuitambulisha huduma mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kuweza kuongeza pesa kwenye kadi zao za mabasi ya mwendokasi kupitia huduma za kifedha ya Airtel Money, akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza huduma mpya itakayowawezesha wateja wake wa Airtel Money kuweza kuongeza pesa kwenye kadi zao za mabasi ya mwendokasi kupitia huduma za kifedha ya Airtel Money

Mpango huu ni sehemu ya juhudu za Airtel kuendelea kutoa huduma za kibunifu zenye gharama nafuu zinazochochea urahisi na usalama katika kufanya malipo katika huduma za usafiri

Meneja wa kitengo cha Airtel Money , Asupya Naligingwa amesema” Tunaamini kwa kuanzia mfumo huu wa kibunifu wa kieletronic katika kufanya malipo kutawahakikishia wakazi wa Dar es salaam usalama, urahisi na uharaka katika kufanya malipo ya huduma za usafiri, lengo letu ni kuhakikisha wateja wetu wananapata urahisi katika kufanya malipo yao mbalimbali ya kila siku ikiwemo kuongeza pesa katika kadi zao za mabasi ya mwendokasi ili kuboresha na kurahisisha safari zao ndani ya jiji”.

Tunaamini kuanzishwa kwa mfumo huu wa malipo kutaleta ufanisi katika huduma za usafiri na maisha ya jamii kwa ujumla kwakuwa kutapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano kwa wasafiri na kuwawezesha kulipia kadi zao kwa urahisi wakati wowote, mahali popote kupitia simu zao za mkononi “ aliongeza Naligingwa

Ili kupata huduma hii mteja anatakiwa kupiga *150*60#, kisha kuchagua 5 kufanya malipo , kisha kuchagua 3 Mwendokasi (DART) na kisha kuingiza kiasi cha pesa, kisha kuingiza reference namba and mwisho kuweka neno la siri kwaajili ya kufanya malipo na kisha mteja atapata ujumbe wa kuthibitisha malipo yake .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: