Sunday, August 14, 2016

YANGA YAIBUKA KIFUA MBELE BAADA YA KUIFUNGA MO BEJAIA BAO 1 - 0

Wachezaji wa Yanga wakishangili goli dhidi ya timu ya MO Bejaia ya Algeria katika Uwanaja wa Taifa Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016 ambapo Yanga iliibuka kifua mbele kwa kuifunga MO Bajaiya bao 1 - 0
Winga wa Yanga kulia, Simon Msuva akipambana na beki wa timu ya MO Bejaia ya Algeria, Zakaria Bencherifa, katika Uwanaja wa Taifa Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa kulia akiwania mpira na beki wa MO Bejaia ya Algeria, Amar Benmelouka, katika Uwanaja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga ilishinda bao1-0.
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa katikati akipambana na mabeki wa timu ya MO Bejaia ya Algeria.
Beki wa Yanga Juma Abdull katika akiwatoka wachezaji wa MO Bejaia ya Algeria,
Kiungo wa Yanga, Yhaban Kamusoko akiwatoka wachezaji wa MO Bejaia ya Algeria,
Wachezaji wa Yanga wakipongezana mara baada ya mpira kuisha.
Mashabiki wakifurahia.
---
BAADA ya Kupata ushindi wa kwanza walioupata Yanga, Koch mkuu wa Hans Van De Pluijm amesema ushindi huu umempa nguvu katika kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe.

Yanga imefanikiwa kushinda goli 1-0 lililofungwa na Mchezaji wa kimataifa kutoka Zimbabwe Thaban Kamosoku dakika ya tatu dhidi ya Mo bejaia mechi iliyofanyika kwenye dimba la uwanja wa Taifa.

Pluijm amesema kuwa, wachezaji wake wamecheza vizuri sana na wameweza kulinda goli katila dakika zote ingawa kuna makosa madogo madogo yaliyojitokeza ila anawapa hongera kwa jitihada walizozifanya.

Naye Nahondha wa Yanga, Vicent Bossou amesema wamefanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha wanatoka ushindi na wamecheza timu nzuri sana yenye uzoefu wa muda mrefu wa michuano ya kimataifa ila anawapongeza pia wachezaji wenzake kwa jitihada walizozifanya.

Baada ya ushindi huo Yanga wanaendea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama nne huku mchezo kati ya Mazembe na Medeama ukitarajiw kuchezwa kesho nchini Ghana.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu