Thursday, September 15, 2016

BANK OF AFRICA (BOA) YAZIDUA KADI MBILI AMBAZO NI TOUCAN VISA NA PROXMA VISA JIJINI DAR

Meneja Masoko, Utafiti na Maendeleo wa Bank of Africa (BOA), Bw. Muganyizi Bisheko akionyesha card aina ya PROXIMA iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.

Benki ya Afrika (BOA) imezindua kadi za TOUCAN VISA CARD na PROXMA VISA CARD zitakazowarahisishia wateja wake kufanya miamala kwenye mashine za kutolea fedha popote duniani. Bw. Muganyizi Bisheko amesema kadi hizo zitawaondolea wateja wao ulazima wa kutembea na pesa nyingi pindi wanaposafiri au wanapofanya manunuzi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Huduma za Kibenki Kidigital wa Bank of Africa (BOA), Bw. Emmanuel Mshindo. Picha na Emmanuel Massaka wa Blogu ya Jamii.
Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Huduma za Kibenk Kidigital wa Bank of Africa (BOA), Bw. Emmanuel Mshindo akionyesha kadi aina ya TOUCAN iliyotolewa na benki ya Afrika (BOA). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo, Bw. Kaisha Boge.
Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo, Bw. Kaisha Boge (katikati) akizielezea kadi hizo zilizotolewa nabenki ya Afrika (BOA) mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu