Wednesday, September 21, 2016

BASI LA SUPER SHEM LAGONGANA NA HIACE NA KUUA WATU 11 MWANZA

Basi la Super Shem baada ya kupata ajali.

Watu 11 wamefariki papo hapo na wengine 7 kujeruhiwa baada ya basi la Super Shem lililokuwa likitokea Mbeya kwenda jijini Mwanza kugongana na daladala (Hiace) katika eneo la Hungumalwa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Diwani wa kata ya Hungumalwa, Shija Malando, amesema ajali hiyo imetokea leo Septemba 21,2016 saa 12 asubuhi baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na daladala iliyokuwa ikitokea kijiji cha Shilima wilayani Kwimba.

Diwani Malando amesema miili ya marehemu pamoja na majeruhi wamepelekwa hospitali ya Ngudu Kwimba na wengine hospitali ya wilaya Misungwi.

Majeruhi wa ajali hiyo waliokuwa kwenye basi wamesema basi lao lilikuwa kwenye mwendo mkali na lilipofika eneo la tukio ghafla daladala hiyo iliingia barabarani na hivyo dereva wa basi kushindwa kuikwepa.

Inaelezwa kuwa waliopoteza maisha na kujeruhiwa ni abiria waliokuwa kwenye daladala.

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu