Sunday, September 25, 2016

BONIFACE JACOB NA MUSTAFA MURO KUGOMBEA UMEYA KINONDONI NA UBUNGO

 
Siku saba baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, Chadema Mkoa wa Dar es Salaam imefanya uchaguzi wa kura za maoni, kujiandaa na uchaguzi wa mameya wa Ubungo na Kinondoni.

Akizungumza baada ya kuvunjwa kwa baraza hilo, Mkurugenzi wa Kinondoni, Aron Kagurumjuli amesema uchaguzi wa kuwapata mameya na manaibu wao unatakiwa kufanyika ndani ya siku 14.

Katika kura za maoni jana, madiwani wa chama hicho wa maeneo hayo waliwapitisha Mustafa Muro kugombea Kinondoni na Boniface Jacob kuwa ni Ubungo.

Kabla ya uchaguzi wa meya, majina hayo yatapelekwa Kamati Kuu ya chama hicho kujadiliwa na kupigiwa kura sanjali na walioshika nafasi ya pili na ya tatu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu