Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya wasusi wa mitindo ya nywele (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la “Msusi Wetu” jana yaliyoanzishwa na kampuni ya Kidoti.
 Mwakilishi wa masuko kutoka Umoja Switch Jasmin Shamshama katikati akizungumzia jinsi watakavyoshiriki katika mashindano ya ususi wa staili mbalimbali za nywele yajulikanayo kwa jina la “Msusi Wetu” jana yaliyoanzishwa na kampuni ya Kidoti.
 Baadhi ya washindani wa mashindano ya  kumtafuta msusi bora wa aina mbalimbali ya nywele yajulikanayo kwa jina la Msusi Wetu wakifuatilia uzinduzi huo.
 Mtangazaji wa kipindi cha  Leo Tena ya Clouds Fm Husna Abdul 'Dahuu' wa kwanza kushoto akizungumza katika uzinduzi huo.

Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo ameanzisha mashindano ya kusuka mitindo mbalimbali lijulikanalo kwa jina la “Msusi Wao’ ambalo ni maalum kwa wasusi ambao hawamiliki vibanda vya saluni.

Shindano hilo linaanza leo Manispaa ya Temeke ambapo washindi watatu watapata zawadi mbalimbali zitakazotolewa na kampuni ya Kidoti kwa kushirikiana na wadau wengine kama Umoja Switch, Abee Naturals na wengine.

Mshindi wa kwanza wa shindano hilo atazawadiwa sh 300,000, nywele za Kidoti zenye thamani ya Sh milioni 1.5 na mashine ya kukaushia nywele ‘Dryer’.

Mshindi wa pili atazawadiwa Sh250,000, nywele za kidoti zenye thamani ya Sh milioni Moja na mashine ya kukaushia nywele ‘Dryer’ na mshindi wa tatu atazawadiwa Sh200,000, nywele za Kidoti zenye thamani ya Sh 500,000 na mashine ya kukaushia nywele ‘Dryer’.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo la kwanza, Jokate alisema kuwa washiriki wanatakiwa kujaza fomu maalum ambazo zinapatikana katika duka la Kidoti lililopo mtaa wa Bonde na Pemba Kariako.

“Msusi anayefanyakazi saluni haruhusiwi kushiriki katika mashindano haya, tutatumia njia mbalimbali kuweza kubaini wasusi ambao wanafanyakazi katika saluni na kuwaondoa, hii ni fursa pekee kwa wasusi ambao wanasukia kwenye vibaraza au vibanda ambavyo siyo rasmi,” alisema Jokate.

Alisema kuwa kutakuwa na majaji watatu katika kila shindano ambao watakuwa chini ya Jaji Mkuu, Conchester Ishengi ambaye ni mtaalam wa masuala ya ususi. Ishengi alisema kuwa watazingatia vigezo vilivyowekwa ili kumpata mshindi.

“Lengo ni kuwawezesha wasusi ambao hawana uwezo wa kupanga vyumba vya saluni, kupitia shindano hili, tutaweza kuwapta wasusi wengi kwani kipaji chako ndiyo utajiri wako,” alisema.

Afisa Masoko wa Umoja Switch, Jasmin Shamshama alisema kuwa wameamua kusaidia shinadno hilo kama sehemu ya kuisaidia jamii kupitia mashindano hayo.

“Tumeandaa ATM kadi za Umoja Switch ambazo si lazima uwe na akaunti, hii unaweza kutumia hata kwa namba yako ya simu, hivyo mashindano ya ‘Msusi Wao’ ni sehemu halisi ya kuwawezesha wajasiriamali,” alisema Jasmin.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: