Tuesday, September 27, 2016

JUMLA YA WATOTO 4000 WANAZALIWA KILA MWAKA NA TATIZO LA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI, TANZANIA

Kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr. Othman Kiloloma akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro sehemu ambayo mtoto amefanyiwa upasuaji wa kichwa.
Mkuu wa wilaya ya Arusha akiwasili katika hospitali ya Mount Meru iliopo jijini hapa Tayari kwakwenda kuangalia watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa.
Kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr. Othman Kiloloma akiwa anampa mkuu wa wilaya ya Arusha maelekezo ya picha inayoonyesha jinsi mtoto alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji.
Na Woinde Shizza, Arusha

Jumla ya watoto 4000 wanazaliwa kila mwaka na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi na kati ya hao ni watoto 500 tu ndio wanafikishwa hospitalini kwa ajili ya upasuaji huku wengine 3500 awajulikani wanapopelekwa.

Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman Kiloloma wakati akiongea na waandishi Wa Habari Mkoani hapa.

Alisema kuwa wao kama taasisi ya moi walikaachini na kuona kunawatoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya garama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho sivyo.

Alibainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 ambayo ni awamu ya kwanza na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.

"Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 atujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu