Thursday, September 15, 2016

KAMBI TIBA YA GSM FOUNDATION YAMALIZA KAZI PWANI, YAELEKEA TANGA

Na Mwandishi Wetu

Wazazi nchini wametakiwa kuwa na moyo wa kujali afya za watoto wao hasa zinapotokea fursa za tiba za bure kwenye jamii zao kwani ni nadra sana kwa fursa hizi kujitokeza katika jamii za kitanzania.

Hayo yamesemwa na mbunge wa Chalinze Mhehimiwa Ridhwani Kikwete alipotembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwana vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Huu ni mkoa wa 10 kwa kambi hii kutembelea, huku ukiwa ni msimu wa tatu wa kambi tiba hizi zenye lento la kuokoa miasma ya watoto takriban 3500 wanaohisiwa kupoteza maisha kila mwaka köa mujibu wa tafiti za MOI za mwaka 2002, ambazo zinasema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka lakeni ni 500 tu huweza kufika kwenye tiba huku changamoto kubwa ikitajwa kuwa ni uchache wa madaktarim ba ukubwa wa gharama za tiba.

Awamu ya kwanza ya kambi tiba ya GSM ilipita mikoa ya Mwanza, Shinyanga. Singida, Dodoma na Morogoro. Ya pili ikapita Mtwara, Songea, Mbeya na iringa. Hii awamu ya tatu itapita katika mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Mara.

PICHANI JUU: Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani - Tumbi, Dk Aggey Geoffey(Wa pili kutoka kushoto), na Dk Silas Msangi( Wa kwanza kushoto), mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha. Kulia ni Afisa uhusiano wa GSM Foundation Khalphan Kiwamba. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Kibaha - Pwani Bi. Chiku mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha - Pwani. Kutoka kulia ni Mkurugeni Mkuu wa GSM Foundation, Shanon na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Tumbi - Kibaha Bw. Dk Aggrey Geoffrey.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na madaktari waliokuwa wakihusika na kuandikisha watoto waliokuwa wakifanyiwa upasuaji.
Mzazi akiwa na mwanae aliyefanyiwa upasuaji.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa nusu Kaputi, Bw. Ogutu Ogonga mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha - Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwashukuru waganga waliotoka GSM Foundation kwa moyo wao wa pekee wa kujitolea kuwafanyia upasuaji watoto hao.
Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani - Tumbi, Dk Aggrey Geoffrey akitoa mrejesho juu upasuaji uliofanyika hospitalini hapo.
Afisa Habari wa GSM Foundation Bw Khalphan Kiwamba akitoa maelezo juu ya upasuaji ulivyofanyika katika Hospitali ya Tumbi - Kibaha. Wanaomsikiliza kutoka kushoto kwenda kulia ni Shannon Kiwamba, Munge wa Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete na Kaimu Mganga Mkuu Aggrey Geoffrey.
Wageni wakiohuduria mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na Mtaalamu wa nusu Kaputi, Bw. Ogutu Ogonga mara baada ya kumaliza zoezi la kukagua kambi hiyo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu