Wednesday, September 21, 2016

KAMPENI YA SIMAMA KAA DESK KUFANYIKA MIKOA YA TABORA NA PWANI ILI KUSAIDIA UPUNGUFU WA MADAWATI

Stella Pius Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kuhusu kampeni ya Madawati mkoani Tabora , katikati ni Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation Bw. Amon Mkoga na kushoto ni Ngo Duy Truong Meneja Masoko Halotel.
Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation Bw. Amon Mkoga katikati, Ngo Duy Truong Meneja Masoko Halotel, Kushoto na Stella Pius Meneja Mawasiliano wa Halotel wakionyesha kwa waandishi wa habari Bango maalum linaloelezea kampeni ya Simama Kaa Desk itakayofanyika mkoani Tabora na Pwani.
---
NA HERIETH HASSAN

Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation Bw. Amon Mkoga ametoa mchango wa madawati katika kampeni ya uchangiaji madawati kwa udhamini wa mtandao wa simu za mkononi wa Halotel hii leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar-es-Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Amon Mkoga amesema kuwa ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ,wameandaa kampeni ya "Simama Kaa Desk" Kampeni., itakayosaidia kupunguza uhaba wa madawati ikidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel.

“Lengo kubwa la kampeni hii ya "Simma Kaa Desk" ni kuchangia na kupunguza upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari ili kumuunga mkono rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Kampeni hiyo itaanzia katika mkoa wa Tabora na Pwani tukiwa pamoja na Kampuni ya Halotel.”

Aidha afisa mawasiliano wa Halotel Stella Pius amesema kuwa Halotel itakuwa pamoja na Dr Mkoga Foundation kuhakikisha kwamba watakuwa bega kwa bega ili kuwasilisha mchango wa madawati katika elimu.

“Ikiwa ni pamoja na kuunga mkono uchangiaji wa madawati Haloteli tutahakikisha katika kampeni hii ya Simama Kaa Desk kampeni, tunawakilisha mchango wetu tukishirikiana na Dr Amoni Foundation kupitia kampeni hii ambapo tunaamini kuwa ni njia pekee ya kupunguza uhaba wa madawati mashuleni.”

Licha ya hayo pia kutakuwa na burudani ya mziki wakati wa kukabidhi madawati hayo ambayo italetwa na kundi la muziki wa kizazi kipya la Mabaga Fresh la jijini Dar es salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu