Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma, Japhar Mwanyemba akipokea moja kati ya madawati 235 yenye thamani ya milioni 39 toka kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, George Lugata. Katikati ni Diwani Kikuyu kaskazini, Israel Mwansasu.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kushoto) Diwani wa Kikuyu kaskazini, Israel Mwansasu na Meya wa Dodoma Mstahiki Japhar Mwanyemba wakiwa wameketi mara baada ya makabidhiano.
Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Patrick Moshi akiongea na walimu,wanafunzi na wanahabari kwenye hafla ya kukabidhi madawati toka kampuni ya Tigo, wengine pichani Meya Japhar Mwanyemba, George Lugata, Aidan Komba.
Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini, Aidan Komba akiongea na walimu, wanafunzi na wanahabari wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati viwanja vya shule ya msingi Kikuyu A mkoani Dodoma.
Walimu na Wanafunzi wakisheherekea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: