Saturday, September 3, 2016

KILOLO FC KUKIPIGA NA TIMU YA WABUNGE MJINI DODOMA


Venance Mwamoto
---
Na Matukiodaima Blog

KOCHA wa timu ya Bunge Venance Mwamoto ametoa mwaliko kwa timu ya Bodaboda Kilolo kwenda bungeni kucheza mchezo wa kirafiki na wabunge

Mwamoto ambae ni mbunge wa Kilolo mkoani Iringa alitoa mwaliko huo wakati wa kikao chake na vijana hao wa bodaboda mjini Ilula Jana.

Alisema kuwa kabla ya kwenda bungeni vijana hao watashindana kupata bingwa wa
mashindano hayo ambaye atakwenda Dodoma kucheza na wabunge

Hivyo alisema lazima kujipanga vema kwa kujiandaa ili kuepuka aibu ya kichapo kutoka kwa wabunge.

"Nawaomba timu itakayoshinda iwe bungeni kutangaza wilaya getu ya Kilolo kisoka pia kuanza rasmi kwa mashindano ya Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia  Abdalah na mimi mbunge wenu nitadhamini "

Hata hivyo alisema kabla ya mashindano hayo atatoa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki kama njia ya kuondoka kero ya vifaa vya michezo.

Mwamoto alisema lengo ni kuona vijana Kilolo wanakuwa na timu na kupitia michezo wanapata ajira kwa kuchezea timu mbali mbali kubwa nchini.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu