Sunday, September 25, 2016

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA ADOLPH SIMON KIVAMWODAR ES SALAAM LEO

Mjane Frigenia (kushoto) na wanawe, Arm Eliza (mwenye miwani) wakiwasili viwanja vya leaders Club.
Wanahabari wakilipokea jeneza baada ya mwili wa marehemu Kivamwo kuwasili viwanja vya vya leaders Club kwa shughuli ya kuagwa.
Mchungaji Reuben Njereka akitoa neno katiba ibada ya kuaga iliyofanyika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo.
Wana habari wakongwe walipata fursa ya kuonana katika tukio hilo. Kulia Muhidini Issa Michuzi 'Ankali' akisalimiana na Bernard Mapalala huku Hamisi Kibari (kushoto) na Charles Kayoka wakitabasamu.
John Holana akisoma risala ya marehemu.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media, Dkt. Reginald mengi akitoa salamu zake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa salam za faraja kwa wafiwa na kuelezea waombolezaji namna bora ya kuenzi mema aliyotuachia marehemu Kivamwo.
Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa mawaidha yake na kusisitiza waombolezaji kutokusahau mazuri yaliyofanya na marehemu Kivamwo na kuaenzi katika maisha yetu..
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) Limited, Dkt. Jim Yonaz akitoa salamu na nasaa zake kwa waombolezaji.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya MCL, Bakari Machumu akitoa pia salam kwa waombolezaji.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, pia Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini, wakili Deodatus Balile akitoa salam zake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akimpa mkono wa pole mjane na watoto wa marehemu.
Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwapa mkono wa pole na watoto wa marehemu.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, pia Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini, wakili Deodatus Balile.
Mhariri Mtendaji wa Mkuu wa New Habari 2006, Absalom Kibanda (kulia) akitoa mkono wa pole kwa wafiwa. Pamoja naye ni Mhariri Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian, Richard Mwigamba.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, pia Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini, wakili Deodatus Balile.
Mjane Frigenia akifarijiwa baada ya kuaga mwili wa marehemu Kivamwo.
Mwana Habari Leah Samike (kulia) na Rechol Mkundai wakiwafariji watoto wa marehemu baada ya kuaga mwili baba yao Adolf Saimon Kivamwo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa sasa na zamani ambao waliwahi kufanya kazi na marehemu Kivamwo kwenye Kampuni ya The Guardian Ltd wakati wa shughuli hiyo.
Askofu Isaya Kiputa wa Kanisa la Pentekoste Holiness Mission akiongoza ibada ya mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam leo.
Mjane Frigenia Adolf Kivamwo akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe.
Wanawe Mariam (kushoto), Amy (mdogo kabisa) na Eliza wakiweka maua kwenye kaburi.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media ambapo marehemu aliwahi kufanyika kazi kwenye Kampuni ya The Guardian Ltd akimwombea marehemu baada ya kuweka shada la maua.
Wabunge Saed Kubenea wa ubungo (kushoto), Zitto Kambwe Kigoma Mjini na Shy-Rose Bhanji wa Bunge la Afrika Mashariki wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Mwenyekiti wa 'Media Car Wash for Cancer' aliyeongoza kampeni ya matibabu ya Kivamwo, Benjamin Thomson na Mwana habari mwenzake Grace Nackso wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Mwana habari Amy Cunningham aliyewahi ufanya kazi na Kivamwo akiweka ua wenye kaburi wakati wa mazishi.
Wana habari wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Wanahabari wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Wanafamilia wakiwa pamoja wafariji wao baada ya mazishi. (Imeandaliwa na robertokanda.blogspot.com).

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu