Kuna nini kimejificha chini ya JAJI MUTUNGI (Msajili wa Vyama vya Siasa -Tanzania) hasa kuhusiana na mvutano baina ya Chama cha CUF na Mwenyekiti aliyeomba yeye mwenyewe kwa hiari yake kuondoka katika nafasi hiyo?

Nani anamsukuma Jaji Mutungi kuwa sehemu ya maamuzi ya ajabu kabisa kuwahi kutokea katika siasa za vyama katika nchi hii, hususan kutaka kumrudisha Lipumba kwenye chama chake kuwa Mwenyekiti wa Taifa?

Leo sitaandika mengi ila nina hofu kuwa unaweza kuwa Mlezi na Mzazi wa watoto unayewafarakanisha, tena kwa kuua nyumba yao? Kwa nini Mlezi anakuwa anaegemea upande mmoja? Kwa maslahi ya nani? Nina mashaka kama Jaji Mutungi ameisoma vema Katiba ya chama cha CUF!!!

Hofu yangu inarejea juu ya uchaguzi uliopita.... Kulikuwa na Mizengwe Zanzibar na Tanzania Bara pia... Huenda CUF na UKAWA walishinda Uchaguzi wa 2015, kwa Pande zote mbili za Serikali Ya Tanzania!!

Visingizio vya usitishwaji wa Mikutano kwa sababu za Usalama na Kiintelijensia ni Koti lililofunika mambo mengi tunayopaswa KUYAHOJI na KUYATAFAKARI nje ya BOKSI.Kuna hofu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake dhidi ya nguvu ya UPINZANI hapa nchini. Hakuna jambo lingine!!

WASSIRA aliwahi kusema: "Kwa nini Serikali haitoi SABABU ya kuahirisha mikutano hadi 2020? Kama ni Nguvu na Mafuriko ya Lowassa kwamba yataathiri shughuli za wananchi hapa nchini, si waseme tu?" (Hii kauli ni nzito na imebeba maono makubwa kwa ambao walitafakari kwa kina).

Steven WASSIRA ni kada anayejua siri nying ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM),hakutamka haya kwa bahati mbaya bali anajua UKWELI wa mambo na Kilichojificha katika Matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 2015!!

Ukiona jitihada kubwa zinafanyika kumrudisha Lipumba ndani ya CUF, mtu aliyefunga virago mwenyewe, ujue kuwa ni Kutaka kuiua CUF na hivyo Kuua Nguvu ya UKAWA kwa Uchaguzi unaokuja 2019(Serikali za Mitaa) na 2020 (Uchaguzi Mkuu). Haya ni maandalizi yanayofanywa chini ya kivuli cha Msajili.

Kwa mtazamo wangu, mimi namchukulia Lipumba kama "Political espionage" Yaani, "Jasusi la Kisiasa" linalokwenda kutekeleza "Mission" maalumu kwa kupandikizwa ndani ya CUF na UKAWA kwa ujumla. Ni hatari kumpokea LIPUMBA katika kipindi hiki ambacho UKAWA wanahitaji kujenga nguvu kubwa zaidi ya Kiuongozi na Mikakati ya Kuiong'oa CCM madarakani.

Rai yangu ni kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kwamba ukiona jambo hilo linafanyika kwa CUF basi mjue kuwa UMOJA wenu Umeingiliwa (DIVIDE AND RULE). Msikubali kuwaachia mchezo huu waucheze CUF peke yao.... BUNDI ameingia nyumbani kwenu Nyote!!

CUF Kaeni imara, msikubali kufanywa "TOILET PAPERS", UKAWA mlitafakari hili kwa kina na kwa mapana!!

KIZAZI CHA KUHOJI

MWENDOKASI UNAUA
Tutafakari kwa hoja kwa Pamoja
Steven Andrew Mmbogo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: