Thursday, September 8, 2016

MGOGORO WA CHAMA CHA CUF WAIVA, KILA MMOJA AKANA KUTOHUSIKA NA KUJIUDHURU KWAKE

 *Prof. Ibrahim Lipumba sihusiki na kujiuzuru kwako.

Akihojiwa na Azam TV Lipumba amenitaja kuwa ndiye niliyemkwaza asirejeshwe kwenye nafasi ya uenyekiti CUF Taifa kwenye mkutano mkuu maalumu uliofanyika tarehe 21/8/2016.

Napenda kukujulisha kupitia UKUTA wangu huu wewe binafsi, wapambe wako na watanzania kwa ujumla. Kwamba madai yake si ya kweli, taratibu zote za kikatiba na kanuni za uendeshaji wa shughuli za chama na vikao vyake zilifuatwa kikamilifu wajumbe 476 waliopiga kura ya kukubali kujiuzuru kwake, wajumbe 14 waliopiga kura za kukataa kujiuzuru kwake, na wajumbe waliobaki wasiozidi 118 walisimama kutaka kuzuia zoezi la upigaji kura lisifanyike kwa kujua kuwa wangeshindwa kupitisha matakwa yao. Hivyo waliendelea kusimama na kuimba nyimbo mbalimbali na kutaka kuzuia shughuli/ajenda za mkutano zisiendelee. Aidha wajumbe wengine kama 65 hawakufanya maamuzi kwa upande wowote. Baadhi ya wajumbe wengine walitoka ukumbini baada ya vijana alikuja nao LIPUMBA ukumbini kuanzisha vurugu.

Ushauri wa bure kwa Prof. LIPUMBA na washabiki wake;

1. Ni kweli kuna baadhi ya wajumbe wana CUF wanakuunga mkono urejee katika nafasi uliyoiacha kwa hiyari yako mwenyewe. Lakini wajumbe na wanaCUF wengi nikiwemo mimi MBARALA MAHARAGANDE Hatukuungi mkono. Dhamira na nafsi zetu zinatusuta kufanya hivyo.

2. Katika mifumo hii ya demokrasia maamuzi ya wengi ndio ufuatwa. Na wachache wanasikilizwa. Zingatia hilo.

3. Katika mazingira haya ya asilimia 80 ya wajumbe wa baraza kuu CUF Taifa wako against you utawezaje kutendakazi zako hata ukirejea?

4. Katika mazingira kama haya ya kumshambulia katibu mkuu wako vipi utaweza kufanya nae kazi?

5. Hoja za kujiuzuru kwako zimekuwa zimebadilika badilika na au kuongezeka mpya siku hadi siku hii inakuwaje? Sasa umejikita katika ubara na uzanzibar hoja na propaganda za MACCM ndizo unazozitumia sasa nani anakutuma kufanya hivi na kwa maslahi yako au yake?
6. Kwanini uheshimu maelekezo ya barua ya msajili inayokuelekeza kuwa msahamilivu? Unatupa kazi vijana wako uliyotulea kisiasa na kutulazimisha tuanze kurekebisha kila unachopotosha.

7. Unaridhia Mashabiki wako kutoa lugha zisizofaa matusi kwa viongozi wenzako?

8. CUF ni taasisi kubwa ya kisiasa nchini siyo chama cha kigodoro. Lazima kuheshimu katiba na taratibu zake.

9. Hakuna katika katiba ya CUF ibara yeyote inayokupa nafasi ya kutengua maamuzi yako ya kujiuzuru.

10. Kwa msingi wa nukta ya 9 hapo juu, kura 476, baraza kuu CUF kukusimamisha uanachama: HAKUNA NAMNA YA KUJINADI KUWA WEWE NI MWENYEKITI HALALI WA CUF, NA KWAMBA UPO NGANGARI KINOMA KULETA VURUGU. Vinginevyo utwambie sasa upo katika episodes II ya move uliyoandaliwa Kigali, Rwanda kuiendeleza... Na umehakikishiwa support na ..................... kutaka kututoa katika ajenda ya kupambana na UKANDAMIZWAJI WA DEMOKRASIA NCHINI. Na madai ya haki ya maamuzi halali ya wazanzibar waliyoyafanya tarehe 25/10/2015.??

11. Hatuna TRUST tena na wewe katika siasa za upinzani nchini. 'Makambwera' mission is aborted and unimplementable for the time being. Umezungurukwa na vijana wenye uwezo mdogo wa kuyafikiria mambo na namna ya kuyatekeleza, wanakupotosha, wamekupeleka kusiko.
UNAPASWA KUJIPANGA upya NA KIVINGINE. ZAMA NA MAJIRA YA KISIASA YAMEBADILIKA SANA.

HATUKUUNGI MKONO JUU YA UCHAFUZI HUU UNAOKUSUDIA KUUFANYA NA WAFUASI WAKO. NA HAKIKA HAMTAFANIKIWA.

Imeandikwa na Maharagande Mbarala. 

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu