Thursday, September 8, 2016

MKUU WA WILAYA YA HANDENI, GODWIN GONDWE ASULUHUSHA MGOGORO WA MPAKA ULIODUMU KWA MUDA MREFU

Mkuu wa wilaya ya Handeni wa kwanzakushoto akisoma ramani ya mwaka 2007 akiwa na viongozi na wananchi ili kujua mpaka upo sehemu gani. Mkuu wa wilaya Mhe. Gondwe amefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa mpaka uliodumu kwa muda mrefu akiwa ameambatana na Wakurugenzi wa halmashauri zote mbili uliohusisha Kijiji cha Kweditilibe cha Handeni vijijini na kitongoji cha makinda kilichopo Handeni Mji.

RAMANI YA 2007 ndiyo iliyotumika kusuluhisha mgogoro huo ambapo aliwaeleza wananchi kuwa ramani hiyo ndiyo iliyotumika kuweka mipaka ya maeneo husika Tanzania nzima na hakuna mwenye mamalaka ya kuibadili isipokua Raisi mwenye mamalaka ya Ardhi ya Tanzania nzima.
Mkuu wa wilaya Mhe. Godwin Gondwe akisalimiana na mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Handeni kabla ya zoezi la kutatua mgogoro wa mpaka.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu