Na Julius S. Mtatiro

Prof. Kitila na wenzako. Sisi sote ni watu wazima na kila mtu ana uzoefu na akili. Itoshe tu kusema kuwa tatizo la CUF litashughulikiwa. Hata kama Msajili, Dola, ACT, CCM watakuwa nyuma ya Lipumba, CUF itashinda vita hii. CUF ingelianza kufanya mambo ya kihuni anayofanya Lipumba leo hii hivi sasa tungezungumza mambo tofauti sana.


Kwani Kitila unadhani hakuna maelfu ya wanachama wa kuvamia ofisi ya CUF, kumtoa Lipumba na kuingiza uongozi unaotambulika na chama? Hao wanachama wapo na wanaomba hata leo waruhusiwe kufanya chochote, wapo kwa maelfu hata hapa DSM, bahati mbaya ni kuwa Lipumba anadeal na watu wanaotaka kufuata taratibu sana, anadeal na sisi tusiohitaji kufanya uhuni n.k. kwa hiyo wewe Kitila na wenzako wachache mtamshangilia sana, kwa sababu mnajua CUF ikipasuka ACT itanufaika, CCM itanufaika na UKAWA itakufa. Lakini nataka ufahamu kuwa sisi ndani ya chama siyo wajinga, tunajua kila kinachoendelea na tunafanya kila kitu kwa kufuata katiba yetu. Mwisho wa mapambano haya ni ushindi mkubwa kwa CUF na si kwa Mtatiro.

Mimi, kwa bahati mbaya sana maishani mwangu, siongozwi na ufuasi. Nilipofika Mkutano Mkuu nilikuwa miongoni mwa wajumbe watatu waliopendekezwa kuwa Mwenyekiti wa Kikao, punde kura zikapigwa na asilimia 75 ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wakanipigia kura niongoze kikao, sikuteuliwa na Maalim Seif. Baraza Kuu lilipokutana baadaye lilinipendekeza kuongoza Kamati ua Uongozi, sikuteuliwa na Maalim Seif, ni Baraza Kuu. Mimi ni mwanasiasa nayekua na kujifunza na bahati mbaya niliyonayo katika maisha yangu ni kuwa kila mara nimekuwa nakabidhiwa majukumu makubwa tena katika nyakati ngumu, lakini mara zote hubezwa na mwisho mimi husimamia misingi na huwa kwenye kundi la washindi.

Mimi ni mwana CUF na hii ni vita ya Lipumba+SYSTEM+ACT+CCM vs THE CIVIC UNITED FRONT. Nataka niwaambie kuwa CUF ndiye mshindi wa vita hii na tukishashinda vita hii njooni mniulize kwa nini niliwahi kusema hivyo.

Tunazo nguvu za kushinda, sababu na rasilimali za kufanya hivyo. Wakati ni Ukuta.

Mtatiro J
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: