Thursday, September 1, 2016

NHC YAWAONDOA WADAIWA SUGU OFISI ZA FREEMEDIA WACHAPISHAJI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA

Katika kutekeleza agizo la wadaiwa sugu, Madalali wa shirika la nyumba la Taifa la - (NHC) mapema leo wamevamia ofisi za Freemedia wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na kutoa vitu.

Mwisho wa mwezi uliopita shirika la nyumba la Taifa - (NHC) kupitia Mkurugenzi Mkuu, Nehemia Mchechu, lilitangaza kuwaondoa wadaiwa wote sugu wanaoishi katika nyumba zao.

KAULI YA MKURUGENZI MKUU WA NHC, NEHEMIA MCHECHU.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi uliopita, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15.

Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanas pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa, Mchechu alisema na kwamba sasa zimesalia wiki tatu.

Alisema baada ya muda huo kumalizika, utekelezaji wa kuondolewa katika majengo hayo utaanza ukiambatana na uchukuaji wa hatua za kisheria.

Mchechu alisema mbali ya Bilicanas, wadaiwa wengine ni Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi inayodaiwa Sh. bilioni mbili, Benki ya Azania (Sh. milioni 161) na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa (Sh. milioni 631).

Wadaiwa wengine walitajwa kuwa ni Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Sh. bilioni 1.3), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sh. bilioni mbili), Tume ya Utumishi (Sh. milioni 109) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sh. bilioni moja.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu