Sunday, September 25, 2016

ONYO; WALE WA KUNUSA NUSA KAZI KWENU, UTAPELI UMEPAMBA MOTO

Kwa wale wakunusanusa ANGALIZO

Kuna utapeli fulani umejitokeza japo ulikuwa wa miaka ya nyuma, umejirudia tena siku hizi.

Kuna matapeli wanatembea na perfumes kumbe mle wamechanganya na spray ya madawa ya kulevya, wanakupulizia kiganjani mwako uinuse kama unavutiwa huku ukijua perfume.

Ukishainusa huchukui dakika 3, unakuwa nusu kaputi, wanasomba kila ulicho nacho, na kama wewe ni mdada, wanamaliza kila kitu na kujilipa disturbance allowance kabisa. Cha msingi achana na perfumes za kutembeza na acha kunusanusa vitu, dunia ishachanganyikiwa hii.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu