Thursday, September 15, 2016

PICHA ZA TUKIO LA KUUNGUA KWA MOTO HOTELI YA KIBAHA CONFERENCE CENTER, KIBAHA - PWANI

 Moto mkubwa umeteketeza baadhi ya majengo ikiwemo jiko na mgahawa wa hoteli ya Kibaha Coference Center (KCC) iliyopo Kibaha, Pwani na kusababisha hasara ya mamilioni.

Akizungumza Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Ukoaji, Goodluck Zelote alisema Moto huo ulianza majira ya saa nane mchana hapo jana Septemba 14, 2016 na kuteketeza baadhi ya majengo hayo.

Alisema kuwa anawashukuru wananchi waliojitokeza kuwasaidia kuzima moto huo ila moto walipata changamoto kubwa kwa vile wakati moto ukiwaka kulikuwa na jua kali lililoendana na upepo mkali na kusababisha kusambaa kwa urahisi zaidi.

Kwa mujibu wa Kamanda Zelote alisema kuwa chanjo cha moto huo kinasaidikiwa ni umeme maana mafundi waliokuwa wakichomelea katika eneo hilo vyombo vyao vilileta viliharibika na kusababisha moto uliyoshika katika makuti na kuanza kuwaka moto.

Aliongeza kuwa ni vyema wananchi kuendelea kutoa taarifa ya majanga ya moto pindi yanapotokea ili kuepusha madhara zaidi.
 
 Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Ukoaji, Goodluck Zeloteakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uzimaji wa moto uliokuwa ukiteketeza hoteli hiyo ya kitaa ya KCC iliyopo Kibaha, Pwani. 
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
 Askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji wakimalizia kuzima moto uliyokuwa umesalia baadhi ya sehemu ya majengo ya hoteli hiyo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu