Friday, September 2, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI PEMBA KWA SAFARI YA KIKAZI

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamewasili leo Septemba 2, 2016 Pemba kwa safari ya kikazi visiwani humo. Rais Dkt. Magufuli amelakiwa na ngoma na shamra shamra.

Ngoma za mapokezi ya rais visiwani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Kisiwa hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Abdallah mara baada ya kuwasili kisiwani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ngoma ya kuyumbizi mara baada ya kuwasili Kisiwani Pemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma Makamu wa Rais wa zamani katika awamu ya Tatu katika kijiji cha Wawi Bigilini kisiwani katika Wilaya ya Chake chake Pemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali kwenye kaburi hilo la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma Makamu wa Rais wa zamani katika kijiji cha Wawi Bigilini kisiwani katika Wilaya ya Chake chake Pemba.
Mama Janeth Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma Makamu wa Rais wa zamani katika kijiji cha Wawi Bigilini kisiwani katika Wilaya ya Chake chake Pemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa mkewe Mama Janeth Magufuli Magufuli wakiomba dua iliyokuwa ikiongozwa na Kiongozi wa dini ya Kiislamu Shekhe Mohamed Suleiman mbele ya kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma Makamu wa Rais wa zamani katika kijiji cha Wawi Bigilini kisiwani katika Wilaya ya Chake chake Pemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli azungumza mara baada ya tukio la uwekaji mashada katika kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma Makamu wa Rais wa zamani katika kijiji cha Wawi Bigilini kisiwani katika Wilaya ya Chake chake Pemba.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea Kisiwani Pemba. Picha na IKULU.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu