Wednesday, September 28, 2016

RAIS MSTAAFU JK MIONGONI MWA VIONGOZI 29 WA KUONGOZA HARAKATI DHIDI TA UTAPIAMLO DUNIANI

(PICHANI: Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon na mjumbe wa jopo Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa Tanzania) Picha UN/Evan Schneider).

Vuguvugu la kuchagiza lishe (SUN) linaendelea na shughuli ya kupigia upatu lishe bora kwa wote, kila mahali, hasa sasa ambapo viongozi wa dunia 29 walioteuliwa wataongeza nguvu ya vita dhidi ya aina zote za utapia mlo.

Viongozi hao walioteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, ni vinara walioahidi kuwdka suala la lishe kama kitovu cha ajenda yao , na kuchagiza na kutoa muongozo kwa vuguvugu la SUN na nia yake ya kutokomeza utapiamlo.

Takwimu za kimataifa zinaonyesha kwamba mtu mmoja kati ya watatu anaugua utapiamlo duniani , na wavulana na wasichana takribani milioni 156 kote duniani wana matatizo ya kudumaa.

Akizungumzia tatizo hilo Ban amesema lishe bora ni muhimu sana katika kufikia ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, na kusema kuna fursa sasa ya kufanya kazi pamoja kubadilisha hali hiyo.

Kundi hilo la viongozi 29 litasaidia juhudi za nchi mbalimbali za kusukuma mchakato wa lishe na kutimiza malengo kwa wavulana, wasichana na familia zao ili kuwe na dunia huru bila utapia mlo ifikapo 2030.

Miongoni mwa viongozi hao walioteuliwa ni Rais wa Guatemala, mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu SDGs, Bwana David Nabarro, Jakaya Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania, na Bwana Akin Adesina, Rais wa benki ya maendeleo ya Afrika. HABARI KWA HISANI YA UN Radio Kiswahili - Redio ya Umoja wa Mataifa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu