Tuesday, September 27, 2016

SECOND BORN, SECOND SON, SECOND PRINCE KARIBU DUNIANI FIDEL/PILATO

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Imeandikwa Jumapili tarehe 25.09.2016 katika historia ya Dunia.

"Kama alivyosema bwana kuwa nitakubariki ukoo wako hadi vizazi na vizazi na huo ndio ukawa mwanzo wa kukua kwa ukoo wa GOGO kutoka UTEGI Rorya Mara.

Ikawa Igogo alizaa wana wa kiume wengi akiwemo Chief Sarungi, naye Chief Sarungi akazaa wana wa kiume wengi akiwemo Leonard Obwago, Naye Leonard Obwago akazaa wana wa kiume 9 ambao ni Martin Lumumba, Boniface Toto, Chief, Morice Kateti, Joseph, Amosi, Edwin Ochacho, Selemani, Peter Oyoko na Daniel Abuka. Naye Peter Oyoko aliyejulikana kama Peter Sarungi akazaa wana wawili wa kiume akiwemo Fidel Pilato.

Nao ukoo wa GOGO ukaongeza maradufu kwa baraka za Mungu"

Namshukuru Mungu kwa Zawadi hii nzuri ya pekee hasa kwa kipindi hiki ambacho majaribu yamenipata kwa wingi lakini hakika Baraka na Rehema za Mungu ni za Milele na wala hata acha mja wake asononeke.

Nampongeza sana Mke na mama wa mtoto Neema Peter Sarungi kwa uvumilivu na ujasiri wa hali ya juu na utayari wa kumleta mtoto dunia. Namwomba amlee mtoto katika malezi ya hekima na busara.

Pia niwashukuru bibi, shangazi na mama zangu wote wakiongozwa na mama yangu Bi Martina Sarungi kwa maombi yao na ushauri wao kwa kipindi chote na nimeona thamani yenu ya kuitwa MAMA.

Pamoja na majina yangu yote kama vile Igwee, Ogaa, Oyoko, Owuonda, Next Spekaer, Peter, Babu wa Bukoba na simba wa Utegi, Sasa unaweza pia kuniita BABA FIDEL ama BABA PILATO.

Asanteni sana.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu