Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo kuzungumzia mpango wa maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) Suleiman Masoud
Meneja Mawasiliamo wa Sumatra, David Mzirai akisisitiza jambo kwenye mkutano huo wa leo na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Mkoani Tanga
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano huo
Waandishi wa Habari wa Mkoani Tanga wakichukua habari leo.
PRO wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga (TPA) Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari wa mkoani Tanga

MAMLAKA ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imekusudia kuanzisha mpango mkakati maalumu wa udhibiti uchafuzi wa mazingira baharini (NMOSCRP) unaosababishwa na umwagaji wa mafuta unaofanywa bila ya kufuata taratibu za mazingira zilizowekwa na kuharibu mazingira.

Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini Taifa Capt Mussa Hamza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wiki ya bahari dunia inayofanyika Kitaifa Mkoani Tanga kwenye viwanja vya Tangamano kesho Jumanne.

Ambapo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yatakayokwenda sambamba na maonyesho mbalimbali na warsha itakayofanyika Septemba 28 mwaka huu.

Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari wame lazimika kuanzisha mpango huo ili kukabiliana na uchafuzi huo ambao unaweza kuchangia utoekaji wa viumbe vya vilivyopo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: