Tuesday, September 20, 2016

WAFANYAKAZI WA GAZETI LA UHURU NA MZALENDO WALIPOYATOA YA MOYONI BAADA YA MWENYEKITI WA CCM, RAIS DK. JOHN MAGUFULI APOFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA OFISI ZAO JIJINI DAR

Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi waliojitokeza katika Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, wakati akitoka Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, katika Mtaa huo, kwenda Ofisi za Kampuni ya Uhuru Publications Limited, Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani jana Septemba 19, 2016. Dk. Magufuli alifika katika ofisi yake leo kufanya kazi zake za kichama kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa CCM.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akifuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili katika Ofisi za Uhuru Publications Limited mtaa wa Lumumba, Da es Salaam, ambako baada ya kutembelea baadhi ya ofisi za kampuni hiyo alizungumza na wafanyakazi ambapo ameahidi kutatua kero zinazowakabili kwa muavuli wake wa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasilikiliza wafanyakazi wa UPL alipowasili katika ofisi hizo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Mkuu wa Kitengo cha kompyuta, wa UPL, Moses Makambi akimpatia maelezo Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipoingia chumba cha Usanifu wa kurasa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiingia katika chumba cha Habari cha Uhuru Publications kuzungumza na wafanyakazi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpatia maelezo ya utangulizi, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji, wa UPL Ramadhani Mkoma.
Wafanyakazi wakiwa ukumbini.
Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini mazungumzo yao na Rais Dk. Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuliu akiandika wakati Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Ramadhani Mkoma akieleza changamoto zinazowakabili wafanyakazi katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Baadhi ya wafanyakazi wakishangilia baada ya Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli kuahidi kushughulikia kero zao kwa nafasi yake ya Ueneyekiti wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Magufuli akimsikiliza Kaimu Mhasibu Mkuu wa UPL huku akinukuu dondoo muhimu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafayakazi wa UPL cha RAAWU, Moses Makambi akieleza changamoto kwa Dk. Magufuli.
Ukumbi wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa UPL na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Magufuli.
Katibu Mkuu wa CCM, akimfafanulia jambo Dk. Magufuli.
Wafanyakazi wakiwa wametulia kufuatilia alichokuwa akisema, Dk Magufuli.
Dk. Magufuli akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL.
Mfayakazi wa UPL Fred Majaliwa akieleza kero anazoona zinakwamisha utendaji wa kazi za UPL.
Rhoda Kangero kutoka Idara ya Rasilimali watu, akieleza kero na changamoto.
Wafanyakazi wa UPL wakimuombea dua Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiondoka ofisi za UPL baada ya kuzungumza na wafanyakazi leo Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na watatu kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshauri jambo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli nje ya Ofisi za UPL. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi kabla ya kuondoka baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa UPL.
Wafanyakzi wa UPL wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli wakati akiondoka. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu