Wednesday, October 26, 2016

DKT MGWATU AWATAKA WATENDAJI KUZIBA MIANYA YA UPOTEVU WA MAPATO TEMESA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) akizungumza na watumishi wa TEMESA Kilimanjaro alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) akiangalia “honing machine” inayotumika kwa ajili ya matengenezo ya vipuli vya magari kituoni hapo, katikati ni Bw Firmin Lyaruu na Meneja Mhandisi wa TEMESA Kilimanjaro Bw. Alfred Ngw’ani.

Na Theresia Mwami- TEMESA Kilimanjaro.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watendaji kuziba mianya ya uvujaji wa mapato, ili kuhakikisha Wakala unakusanya mapato iliyokusudia na kufanya matumizi stahiki kwa maendeleo ya Wakala.

Amesema hayo wakati akizungumza na na watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanajaro alipotembelea na kujionea hali ilivyo katika kituo hicho na kuwahimiza watumishi wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na kutoa huduma zenye ubora.

“Nawaomba muwe na mbinu mbadala yakuzuia mianya ya uputevu wa mapato na mzibane Taasisi mnazozidai walipe madeni ili mapato yatakayokusanywa yasaidie kuboresha zaidi karakana zetu.” Alisisitiza Dkt. Mgwatu.

Nao watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanjaro kwa nyakati tofauti, wamemuahakikishia mtendaji huyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzidi kupambana kuipeleka mbele TEMESA ingawa kumekuwapo na ukosefu wa vitendea kazi kulingana na taaluma mbali mbali zilizopo kwenye kituo hicho.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu