Baadhi ya vijana wakijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi –NEC (Kulia) waliokuwa wakitoa Elimu ya Mpiga Kura wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana mkoani, wilayani Bariadi, Simiyu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea kutoa Elimu ya Mpiga kura nchini kwa kukutana na wananchi wa makundi mbalimbali.
Afisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Hubert Kiata akitoa elimu ya Mpiga kura kwa wakazi wa wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Bariadi waliojitokeza kupata Elimu ya Mpiga Kura iliyokuwa ikitolewa na Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mkoani Simiyu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha programu endelevu za kuwafikia wananchi moja kwa moja kuwapatia elimu ya mpiga kura kupitia mikutano, maonesho mbalimbali na vyombo vya habari.
Maofisa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Hurbert Kiata (kulia) na Upendo wakisikiliza kwa makini Hoja na maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na vijana wa wilaya ya Bariadi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Taratibu na Sheria zinazosimia Chaguzi za Tanzania. Picha/Aron Msigwa –NEC.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: