Wednesday, October 19, 2016

MANTRA KUANZA UZALISHAJI URANI


Makamu wa Rais wa Operesheni za Kampuni ya Uranium one, Andua Shutor, akizungumzia uchimbaji wa madini ya Urani katika Mradi wa Mkuju, Ruvuma. Wengine ni Makamu wa Rais wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Rosatom, Vladmir Hlavinka na Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania, Frederick Kibodya.
---
UCHIMBAJI wa madini ya Uranium unatarajiwa kuanza rasmi ndani ya miaka miwili, kwa kutumia teknolojia ya kisasa isiyohitaji kuchimba udongo katika eneo la mradi iitwayo In-Situ Recovery (ISR).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makamu wa Rais anayeshughulikia maendeleo kimataifa katika kampuni ya Rosatom inayosimamia uchimbaji wa madini yayo muhimu, Vladmir Hlavinka alisema uchimbaji huo unatarajiwa kuanza baada ya kukamilika kwa taratibu zote za awali za utafiti.

Hlavinka alisema teknolojia hiyo mpya isiyohusisha ubomoaji wa ardhi na uchumbaji wa udongo itaanza kutumika nchini kwa kutoboa shimo la karibu futi moja kisha kumwaga kimiminika kitakachozama ardhini hadi kufikia eneo lenye madini hayo.

“Teknolojia hii ya kisasa ni ya aina yake, ni teknolojia rafiki sana wa mazingira ambayo itasaidia kuifikia urani na kuitoa ardhini bila kuwa na mabaki ambayo yatahitaji kuteketezwa na kusababisha athari za mazingira,” alisema.

Alisema kampuni hiyo inayoendesha uchimbaji wa urani nchini Marekani, Kazakhstan na katika mto Mkuju uliopo Ruuvuma nchini Tanzania inatarajia kuzalisha ajira zinazofikia 1600 hadi mradi hu utakapokamilika.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mantra Tanzania, Frederick Kibodya alisema kampuni hiyo ya Uranium One iliyopo chini ya kampuni ya Rosato ya Urusi imekuwa na ufanisi wa hali ya juu katika shughuli hizo za uchimbaji wa urani na imetekeleza wajibu wake vyema katika utafiti wake wa miaka mitano iliyopita.

Alisema miongoni mwa faida zinazotarajiwa baada ya kuanza kuzalishwa ni kuongeza mapato ya serikali, kuinua uwekezaji wa zaidi ya Dola bilioni moja za Marekani, kuzalisha ajira, uwekezaji katika teknolojia mpya na kutoa fursa kwa wazalishaji wa ndani kuuza bidhaa zao.

Alisema faida za muda mrefu ni uhakika wa urutubishaji wa Urani kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, teknolojia yenye uhakika zaidi hasa katika kuwezesha mpango wa serikali za uwekezaji katika viwanda na kuingia katika uchumi wa kati.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu