Naibu waziri wa afya maendeleo ya Jamii Dkt. Khamis Kigwangala anatarajia kuwa mgeni Rasmi katika Matembezi ya Hisani katika kuhamasisha Uchunguzi wa kuchangia Tiba ya Saratani ya Matiti.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Ripoti toka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya saratani ya Ocean Road Julius Mwaisegile amesema kuwa matembezi hayo yanatarajia kufanyika Oktoba 29 na yana lengo ya matembezi hayo ni kuongeza uelewa wa saratani ya matiti.

Aidha ripoti hiyo ilisema kwamba ipo haja kwa jamii kuchangia juhudi za serikali katika kuimarisha tiba ya saratani ya matiti hivyo fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba, Dawa za dripu zinahitajika ili kuondokana na changamoto hizo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: