Friday, October 7, 2016

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA

Katibu Msaidizi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ofisi ya Kanda Dodoma, Bw. Cathlex Makawia (aliyesimama kushoto) akimuapisha Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Erasto Aron Mfugale (kulia) leo Oktoba 7, 2016 aliyeteuliwa kushika wadhifa huo Oktoba 3, 2016.
Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Bw. Erasto Aron Mfugale akila Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Oktoba 7, 2016 katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma – Dodoma kushika nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Steven Kamkonda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Septemba 27, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kubainika kufungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu