Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba kasema kitendo cha CHADEMA kushindwa katika uchaguzi wa Umeya wa Kinondoni unatokana na ubinafsi mkubwa.

Lipumba kasema tokea awali alishauri mgombea wa umeya angetokana na chama cha CUF na sio CHEDEMA. “Kama sio ubinafsi na umangimeza wa rafiki zangu Chadema, upinzani tungeshinda hicho kiti” Lipumba.

Lipumba kazidi kusema kuwa CUF ndio chama pekee kinachokubalika kwa Kinondoni. Na ndio maana hata mbunge wake ni wa CUF. Sasa hawa ndugu zangu wameleta ubinafsi mkubwa mpaka wameshindwa.

Mwenyekiti huyo kasema hayo katika ziara yake inayoendelea mkoa wa Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: